Search This Blog

Thursday, April 3, 2014

CHAKULA CHANGU PICHA ZANGU


Hallo, Natumaini  wote ni wazima na Asante kwa kutembelea blog yangu. Sijawahi kupost kuhusu mambo ya jikoni ila leo nimeona ni post baadhi ya picha nilizonazo katika maktaba yangu kuhusu vyakula nilivyowahi kuandaa.


Mimi huwa napenda kupiga picha  chakula changu kabla sijakila. Iwe ni matunda, juisi, vitafunwa au chochote kile nikimaliza kuandaa picha inafuata. Kupiga picha ni kitu  kimojawapo ninachokipenda na mambo ya misosi pia napenda, kwa hiyo napenda kupiga picha vyakula sababu najivunia kazi niliyoifanya kuandaa chakula hicho, kuweka kumbukumbu  pia ni kitu muhimu.Napenda kupika, ila napendelea zaidi kupika vyakula ambavyo ni rahisi na havichukui muda mwingi.     Wewe Je, Ungependa kutwambia kwa nini una piga picha vyakula na kushare picha hizo katika mitandao ya kijamii? Karibu


Ni hayo tu kwa sasa, nakukumbusha kula vizuri ni muhimu  kwa afya yako, kula  matunda matano kwa siku aina tofauti na mboga za majani, kunywa maji ya kutosha na mazoezi ni muhimu hata nusu saa kwa siku. Siku njema.