Search This Blog

Tuesday, June 3, 2014

ORANGE LEMON JUICE RECIPE


Hi, mimi huwa napenda  sana juisi ya machungwa sababu ni tamu na ni rahisi sana kutengeneza, kwa wanaopenda juisi kama mimi watakubaliana na hili. Haya twende kwenye topiki yetu, juisi hii nitakayokwenda kuielezea jinsi ya kutengeneza ni natural, yani hauongezi kitu chochote, maji wala sukari.                           Orange Lemon Juice Recipe
Muda: 10-20 minutes, kwa watu wawili

        Mahitaji

  • Machungwa makubwa 4
  • Limao nusu
                              Jinsi ya kutengeneza
  • osha machungwa yako na ndimu

  • Tayarisha orange squeezer yako ya mkono au umeme   • Kamua machungwa  na ndimu kwa kutumia squeezer

  • Ukimaliza chuja juisi yako na mimina katika glass weka ice cubes na itakuwa tayari kwa kunywa.


 

 
 
Juisi hii unaweza kuinywa wakati wowote  utakaopenda iwe breakfast au lunch.
 
                  
                               Zingatia
  •   ndimu nyingi utaifanya juisi kuwa chungu au kali zaidi  kama unainywa ikiwa natural.


  • Weka ice cubes pale unapokuwa tayari kuinywa juisi yako, ukiweka mapema zitayeyuka na kuwa kama umeongeza maji.