Search This Blog

Wednesday, June 18, 2014

VEGETABLE SALAD RECIPE

 

 
 
Hii ni salad niliyotengeneza jumanne, ni mchanganyiko wa mboga tano; vitunguu, tango, karoti, hoho  na nyanya kisha nikakamulia ndimu. Napenda sana kutengeneza salad hii sababu  ina virutubisho tele, pia ni tamu ( nutritious and delicious) na rahisi sana kuitengeneza.

                               VEGATABLE SALAD RECIPE

Muda: dakika 15-30
           Kwa watu 3

Mahitaji


 • Nyanya  kubwa 2
 • Vitunguu vikubwa 2
 • Karoti kubwa 2
 • Hoho kubwa 1
 • Tango kubwa 1
 • Ndimu 1
 • Chumvi kijiko cha chai robo

Jinsi ya Kutengeneza
 • Osha vizuri mboga  na maji ya moto kiasi na ziache zichuje maji

 • Tayarisha bakuli ya kuwekaa salad
 • Kata vitunguu vipande vidogo na weka katika bakuli, endelea kukata tango, nyanya, karoti na hoho na unaweka vyote katika bakuli, unaweza kutumia kisu au grater kukatia.

 • Tia chumvi na changanya salad taratibu

 • Kisha kamua ndimu yako na itie katika salad, hapo salad yako itakuwa tayari kuliwa


Mengineyo

 
 • Salad hii unaweza kuitumia kama appetizer salad, kuongeza appetite yako (as the first course of a meal)
 • Pia unaweza kuitumia kwenye main course  as side dish, unaweza kulia na pilau au ndizi na nyama choma nk.