Search This Blog

Sunday, August 24, 2014

TAMARIND JUICE RECIPE ( JUISI YA UKWAJU)

Hi, leo nimeona ni share nanyi jinsi ya kutengeneza juisi ya ukwaju, ni rahisi na pia juisi ya ukwaju ni tamu sana.
 

                         TAMARIND JUICE RECIPE
Mahitaji:
 • Ukwaju 450 G
 
 • Sukari, kiasi unachotaka
 • Ndimu robo
 • Maji 2.5 liters
 
                           JINSI YA KUTAYARISHA 
 • Osha ukwaju vizuri kisha uache uchuje maji
 
 • Ondoa maganda ya ukwaju
 
 • Weka ukwaju katika sufuria Tia maji na sukari, weka sufuria jikoni washa moto na uache uchemke kwa dakika kumi , zima jiko na ukoroge hadi uchaanganyike vizuri.
 
 • Kisha uache hadi upoe kabisa na uchuje , kisha kamulia ndimu kuongeza ladha.
 
 
 • Weka katika jug kisha weka katika fridge ipate baridi, baada ya hapo juisi yako ya ukwaju itakuwa tayari kwa kunywa.
 
Mengineyo;
 • Ndimu siyo lazima, maana mimi nimetumia ukwaju mtamu (sweet tamarind) wa Thailand, ndio maana nimeweka, ukitumia ule wa kitanzania au African tamarind tayari ukwaju wenyewe ni mchachu.
 • Unaweza ukanywa juisi na  chakula chochote unachopenda.